Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 24

Ar-Ra'd 13:24

الرعد

سَلَـٰمٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ ۚ فَنِعْمَ عُقْبَى ٱلدَّارِ

Maana

(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu), kwa sababu ya vile mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera. [24]

[24] Hizo Roho zitawaambia: Amani ya milele ni yenu kwa sababu ya kuvumilia kwenu maudhi, na kusubiri kwenu katika kupambana na matamanio yenu. Ni mazuri mno haya malipo mnayo yapata, nayo ni kupata makaazi katika Nyumba ya Neema ya Peponi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Malaika watawaambia, «Amani iwashukie, yakiwa ni maamkizi yenu peke yenu, na msalimike na kila baya kwa uvumilivu wenu katika kumtii Allah Mtukufu. Neema ya nyumba ya mwisho ni Pepo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net