Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 23

Ar-Ra'd 13:23

الرعد

جَنَّـٰتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنْ ءَابَآئِهِمْ وَأَزْوَٰجِهِمْ وَذُرِّيَّـٰتِهِمْ ۖ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ

Maana

Nazo ni Bustani za milele, wataziingia wao na wale waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika watawaingilia katika kila mlango.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na walio wema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango. [23]

[23] Hayo ndiyo malipo mema, ya ukaazi wa moja kwa moja katika Bustani za neema. Watakuwa wao humo pamoja na wazazi wao walio kuwa njema Imani yao na a'mali yao. Pamoja nao pia watakuwa na wake zao na dhuriya zao (wazao wao). Na Roho Safi zitawasalimu na kuwaingilia kila upande.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwisho wao ni mabustani ya Pepo ya ‛Adn, watakaa humo, hawatatoka humo, na pamoja nao watakuwamo waliokuwa wema miongoni mwa mababa, wake na watoto waume kwa wake, na huku malaika wakiingia kwao kwenye kila mlango wakiwapongeza kwa kuingia Peponi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net