Ar-Ra'd 13:22
الرعدوَٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُوا۟ مِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِٱلْحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عُقْبَى ٱلدَّارِ
Na ambao husubiri kwa kuutaka uso wa Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa katika vile tulivyowapa, kwa siri na kwa uwazi, na wanayaondoa mabaya kwa mazuri. Hao ndio wana malipo ya nyumba nzuri ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashika Swala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya Akhera. [22]
[22] Na wanavumilia maudhi wakitafuta radhi za Mwenyezi Mungu iwasaidie katika Njia ya kuwania Haki. Wanashika Swala kama inavyo pasa kusafisha roho zao, na kumkumbuka Mola wao Mlezi. Na wanatoa kutokana na mali aliyo wapa Mwenyezi Mungu kisirisiri na kwa dhahiri bila ya kutaka kuonyesha watu, na kwa maovu wanao tendewa wao wanalipa mema. Na wao kwa sifa hizi watapata malipo mema kwa kukaa katika ahsani ya nyumba, nayo ndiyo Pepo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nao ndio ambao walivumilia udhia na kusimama juu ya utiifu na kujiepusha na uasi kwa kutafuta radhi za Mola wao, walitekeleza Swala kwa namna iliyotimia zaidi, walitekeleza Zaka za lazima za mali yao na matumizi yanayopendekezwa kwa siri na kwa dhahiri na wakawa wanaondoa baya kwa zuri lenye kulifuta. Hao wanaosifika kwa sifa hizi watakuwa na mwisho wenye kusifiwa huko Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net