Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 21

Ar-Ra'd 13:21

الرعد

وَٱلَّذِينَ يَصِلُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيَخَافُونَ سُوٓءَ ٱلْحِسَابِ

Maana

Na wale ambao huyaunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanamhofu Mola wao Mlezi, na wanaiogopa hesabu mbaya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya. [21]

[21] Hao ni Waumini; ada yao ni mapenzi na ut'iifu. Hao wanaamini mapendo baina ya watu, na wanahurumia jamaa zao, na wanawasaidia wenzi wao katika Haki, na wao wanaijua Haki ya Mwenyezi Mungu, na wanaiogopa hisabu ya kuwachusha Siku ya Kiyama, na kwa hivyo wanajikinga na madhambi kwa kadri wawezavyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nao ndio ambao wanawaunga wale ambao Allah Mtukufu Amewaamrisha wawaunge kama jamaa wa karibu na wahitaji, wanamuabudu Mola wao na wanaogopa kupata hesabu mbaya kwa madhambi yao yote na Asiwasamehe chochote katika hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net