Ar-Ra'd 13:20
الرعدٱلَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهْدِ ٱللَّهِ وَلَا يَنقُضُونَ ٱلْمِيثَـٰقَ
Wale ambao wanatimiza mapatano yao na Mwenyezi Mungu, wala hawavunji agano.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji maagano. [20]
[20] Hao ndio wanao tambua Haki. Wao ndio wanao timiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyo juu yao kwa muujibu wa maumbile, na kwa muujibu wa maagano yao na ahadi zao walizo fungamana nazo; wala hawavunji maagano walio fungamana nayo kwa jina la Mwenyezi Mungu baina yao na waja wenzi wao, na kwa maagano makubwa walio jifunga nayo kwa maumbile yaliyo wafanya waitambue Haki na waamini, isipo kuwa walipo jipoteza wenyewe nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ambao wanatekeleza ahadi ya Allah Mtukufu Ambayo Aliwaamrisha kwayo na hawaitengui ahadi ya mkazo ambayo walimuahidi nayo Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net