Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 19

Ar-Ra'd 13:19

الرعد

أَفَمَن يَعْلَمُ أَنَّمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ٱلْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَىٰٓ ۚ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ

Maana

Je, anayejua ya kwamba yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Hakika wenye akili ya hali ya juu tu ndio wanaokumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Anaye jua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Wenye akili ndio wanao zingatia, [19]

[19] Hakika walio ongoka na walio potoka hawawi sawa. Basi je, anaye jua ya kuwa uliyo teremshiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliye kulea akakuumba akakuteuwa kufikisha ujumbe wake, kuwa ni Haki isiyo na shaka yoyote...je huweza kuwa huyo kama aliye potea akaitupa Haki, hata akawa kama kipofu? Hakika hawatambui Haki wakazingatia utukufu wa Mwenyezi Mungu, ila watu wenye akili ya kufikiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, yule anayejua kwamba kile ulichokuja nacho, ewe Mtume, ndicho ukweli unaotoka kwa Allah Mtukufu na akauamini ni kama kipofu asiyeuona ukweli ambaye hakuamini? Hakika wanaowaidhika ni wenye akili timamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net