Ar-Ra'd 13:18
الرعدلِلَّذِينَ ٱسْتَجَابُوا۟ لِرَبِّهِمُ ٱلْحُسْنَىٰ ۚ وَٱلَّذِينَ لَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُۥ لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفْتَدَوْا۟ بِهِۦٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ سُوٓءُ ٱلْحِسَابِ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ
Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata mazuri. Na wale ambao hawakumuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea! Hao wana hesabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni mahali pabaya mno pa kupumzikia!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walio muitikia Mola wao Mlezi watapata wema. Na wasio muitikia, hata wangeli kuwa navyo vyote viliomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikombolea! Hao watapata hisabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahala pabaya mno! [18]
[18] Watu kwa mujibu wa kupokea kwao uwongofu ni mafungu mawili. Fungu moja lilio itikia wito wa Mwenyezi Mungu Muumba Mwenye kupanga. Hilo litapata malipo mema duniani na Akhera. Fungu jengine lisilo itikia wito wa Aliye waumba. Hawa watapata malipo maovu Akhera. Na lau kuwa wanamiliki kila kiliomo duniani na mfano wake mara ya pili, hawawezi kujikinga na hayo malipo maovu! Lakini watapata kumiliki hayo? Kwa hivyo yao wao ni hisabu ya kuwaudhi, na wataishia katika Jahannamu, na huko ni pahali paovu mno pa kuishi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Pepo ni ya wenye kuamini ambao wanamtii Allah Mtukufu na Mtume Wake, na Moto ni wa wale ambao hawakumtii na wakamkanusha. Na lau wangekuwa wanamiliki kila kilichoko ardhini na zaidi ya kama hicho pamoja nacho, wangalikitoa kwa kujikomboa nafsi zao na adhabu ya Allah Mtukufu Siku ya Kiyama, na hakingalikubaliwa kutoka kwao. Wao watafanyiwa hesabu kwa kila tendo baya walilolitenda. Na makazi yao ya kukaa ni Jahanamu, itakuwa ni tandiko kwao. Na tandiko baya mno ni hilo walilojitayarishia nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net