Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 3

Ar-Ra'd 13:3

الرعد

وَهُوَ ٱلَّذِى مَدَّ ٱلْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَٰسِىَ وَأَنْهَـٰرًا ۖ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ ٱثْنَيْنِ ۖ يُغْشِى ٱلَّيْلَ ٱلنَّهَارَ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Maana

Naye ndiye aliyeikunjua ardhi na akaweka humo milima mathubuti na mito. Na katika kila matunda akafanya jozi, cha kiume na cha kike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kaumu wanaotafakari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. [3]

[3] Na Subhanahu, Mwenyezi Mungu Aliye takasika, ndiye aliye kukunjulieni ardhi, akaidhalilisha ili muweze kutembea juu yake mashariki na magharibi. Na Yeye akajaalia katika hii ardhi milima iliyo simama imara, na mito ya maji matamu inayo miminika. Na akajaalia kwa hayo maji matunda ya kabila mbali mbali yanayo zaliana, na kati ya kabila hizo namna mbali mbali, mengine matamu na mengine makali, mengine meupe, na mengine meusi. Na Yeye Subhanahu huufunika mchana kwa usiku. Na hakika katika huu ulimwengu na ajabu zake zimo alama wazi za kuthibitisha uwezo wa Mwenyezi Mungu na Umoja wake kwa anaye fikiri akazingatia. Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia katika kila mimea dume na jike ili ipate kupandishika sehemu ya uke kwa chembe za uzazi zilioko katika sehemu za ume. Na kwa hivyo ndio huzalikana namna kwa namna na kwa wingi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Ambaye Aliifanya ardhi iwe kunjufu iliyonyoshwa, Akaitayarisha kwa maisha yenu, Akayaweka humo majabali yenye kuithibitisha na mito ya nyinyi kunywa na kunufaika, Akaweka humo aina mbili za kila matunda, katika hayo kukawa kuna meupe na meusi, tamu na kali, na Akaufanya usiku ufunike mchana kwa giza lake. Hakika katika hayo yote pana mazingatio kwa wenye kuyafikiri wakawaidhika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net