Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 2

Ar-Ra'd 13:2

الرعد

ٱللَّهُ ٱلَّذِى رَفَعَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِى لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ يُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ

Maana

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua juu mbingu bila ya nguzo mnazoziona, kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi, na akatiisha jua na mwezi, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Anaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona, ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt'ii, kila kimoja kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na Mola wenu Mlezi. [2]

[2] Hakika aliye kiteremsha hichi Kitabu ni Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye aliye zinyanyua hizi mbingu mnazo ziona zenye nyota zipitazo bila ya nguzo mnazo ziona, wala hazijui mtu ila Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa amezifunganisha hizo na ardhi kwa funganisho zisio katika ila akipenda Mwenyezi Mungu. Na amedhalilisha jua na mwezi chini ya Ufalme wake na kwa ajili ya manufaa yenu. Na jua na mwezi yanazunguka kwa mpango maalumu kwa muda alio ukadiria Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la. Na Yeye Subhanahu anapanga kila kitu katika mbingu na ardhi, na anakubainishieni Ishara zake za kuumba kwa kutaraji mpate kuamini kuwa Yeye ni Mmoja wa pekee.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Aliyetukuka Ndiye Aliyeziinua mbingu saba kwa uwezo Wake bila ya nguzo, kama vile ambavyo mnaziona, kisha akawa juu ya arshi yake kulingana na utukufu Wake na ukubwa Wake, na Akalidhalilisha jua na mwezi kwa manufaa ya waja, kila moja wapo ya viwili hivyo kinazunguka kwenye anga lake mpaka Siku ya Kiyama. Anaendesha, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, mambo ya ulimwenguni na Akhera, Anawafafanulia dalili zenye kuonyesha uwezo Wake na kwamba yeye hakuna mungu isipokuwa Yeye, ili muwe na Imani ya kikweli kwa Allah Mtukufu na muwe na yakini ya kurudi Kwake, mpate kuamini ahadi Yake ya thawabu na adhabu na mumtakasiye ibada Peke Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net