Ar-Ra'd 13:1
الرعدالٓمٓر ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ۗ وَٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ٱلْحَقُّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ
Alif Laam Miim Raa.[1] Hizi ni Ishara za Kitabu. Na yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Miim Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Alif Lam Mym Ra. (A.L.M.R.) Hizi ni Ishara za Kitabu. Na uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini. [1]
[1] "Alif Mym Ra" hizi ni harufi za kutamkwa zimeanzia baadhi ya Sura za Qur'ani. Nazo zinaashiria kuwa huu ni muujiza juu ya kuwa ni harufi wanazo zitumia Waarabu katika maneno yao ya kawaida! Na harufi hizi zilikuwa zikitamkwa huwavutia Waarabu waisikilize Qur'ani! Kwani wale mapagani (washirikina) waliambizana wasiisikilize hii Qur'ani. Ikawa Waumini wakianzia harufi hizi huvutia masikio ya washirikina wakawa wanasikiliza. Hakika hizo Aya au Ishara tukufu ndio hii Qur'ani, Kitabu chenye shani kubwa, uliyo teremshiwa wewe Nabii kwa haki na ukweli kutokana na Mwenyezi Mungu, aliye kuumba, na akakuteuwa. Lakini wengi wa washirikina walio yakanya yaliyo kuja ya Haki si watu wa kuikubali Haki. Bali wao wanaipinga kwa inda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alif, Lãm, Mîm. Maelezo kuhusu herufi ziliokatwa na kutengwa yametangulia mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.Hizi ni aya za Qur’ani zenye cheo kitukufu. Na Qur’ani hii uliyoteremshiwa, ewe Mtume, ndiyo haki, na sivyo kama vile wanavyosema washirikina kwamba wewe mwenyewe ndio uliyoileta. Pamoja na hili, wengi wa watu hawaiamini wala hawaifuati kivitendo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net