Yusuf 12:111
يوسفلَقَدْ كَانَ فِى قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَىٰ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ ٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَىْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Hazikuwa hadithi tu zilizozuliwa, bali ni za kusadikisha yale yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kina wa kila kitu, na ni uongofu na rehema kwa kaumu inayoamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Si maneno yaliyo zuliwa, bali ni ya kusadikisha yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu yenye kuamini. [111]
[111] Na Sisi tumekufunulia tuliyo kufunulia katika visa vya Manabii ili kuuthibitisha moyo wako, na iwe ni hidaya kwa watu wako. Na tumetengeneza mazingatio na waadhi wa kuwanawirisha wenye akili na busara, na wanao tambua kuwa Qur'ani ni haki na kweli. Hizi hazikuwa ni hadithi za kutunga, wala nganu za kuzua. Bali hakika ni kweli na ufunuo, wahyi, wenye kuhakikisha ukweli wa yaliyo pita katika Vitabu vya mbinguni, na walio kuja nayo Mitume wengine! Na zinabainisha yanayo hitaji kufafanuliwa katika mambo ya Dini, na zinaongoa kwendea katika Haki na Njia Iliyo Nyooka, na zinafungua milango ya rehema ya Mwenyezi Mungu ili aongoke mwenye kufuata uwongofu wake, na akawa miongoni mwa Waumini wa kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika kwenye habari za Mitume tulizokuelezea na mambo yaliyowakumba wenye kukanusha kuna mawaidha kwa wenye akili timamu. Hii Qur’ani haikuwa ni habari ya urongo iliyozuliwa, lakini tumeiteremsha ikiwa ni yenye kutolea ushahidi ukweli wa vitabu vilivyoteremshwa vilivyotangulia na kwamba vinatoka kwa Allah Mtukufu, na ikiwa ni ufafanuzi wa kila ambalo waja wanalihitaji la kuhalalishiwa na kuharamishiwa, linalopendeza na linalochukiza na mengineyo, na ikiwa ni muelekezo kutoka kwenye upotevu na ni rehema, kwa wenye Imani, ya kuzifanya nyoyo zao ziongoke, wapate kuyafuata kivitendo maamrisho na makatazo yaliyomo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net