Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 110

Yusuf 12:110

يوسف

حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسْتَيْـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا۟ جَآءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّىَ مَن نَّشَآءُ ۖ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْمُجْرِمِينَ

Maana

Mpaka Mitume walipokata tamaa (ya watu wao kuamini) na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, kwa hivyo wakaokolewa sawasawa tuwatakao. Na adhabu yetu haiwezi kurudishwa dhidi ya kaumu wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya wakosefu. [110]

[110] Ewe Muhammad! Wala usione nusura yangu inakawia, kwani nusura yangu ipo karibu na hakika inakuja. Na Sisi tuliwatuma kabla yako Mitume, na kwa mujibu wa hikima yetu msaada wetu ulikawilia. Na wao wakawa wanaendelea kukanywa na watu wao, mpaka nafsi zilipo tikisika, wakahisi kukata tamaa, nusura yetu ikawadiriki; tukawaneemesha kwa kuwaokoa na kuwaletea amani wale walio stahili kutaka uwokofu kwetu, nao ni Waumini. Tukawageuzia maovu wale walio tenda dhambi kwa inadi na wakashikilia ushirikina. Wala hapana awezae kuizuia adhabu yetu isiwafikie watu wakosefu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usiwe na haraka, ewe Mtume, ya kupata ushindi juu ya wanaokukanusha, kwani Mitume kabla yako hawakuwa wakijiwa na ushindi wa haraka kwa hekima tunayoijua. Ifikapo hadi Mitume kukata tamaa na watu wao na kuwa na hakika kwamba watu wao wamewakanusha na hakuna tamaa ya wao kuamini, ushindi utawajia wakati ambapo shida imezidi, basi hapo tuwaokoe tunaowataka kati ya Mitume na wafuasi wao. Na adhabu yetu haitorudishwa kutoka kwa Aliyefanya uhalifu na akamfanyia ujasiri Allah Mtukufu. Katika hili kuna kumliwaza Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net