Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 109

Yusuf 12:109

يوسف

وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ ٱلْقُرَىٰٓ ۗ أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۗ وَلَدَارُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Maana

Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia ufunuo (wahyi) miongoni mwa watu wa mijini. Je, hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo bora kwa wamchao Mungu. Basi hamtumii akili?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipo kuwa wanaume tulio wafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je! Hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ni bora kwa wamchao Mungu. Basi hamfahamu?. [109]

[109] Wala Sisi hatukuacha mtindo wetu katika kuwateuwa Mitume tulipo kuteuwa wewe, ewe Nabii! Wala hali ya kaumu yako haikuwa mbali na hali ya kaumu nyengine zilizo tangulia. Kwani hatukuwateuwa Malaika kabla yako, bali tuliwateuwa wanaume wanaadamu katika watu wa mijini, ukawateremkia Ufunuo, yaani Wahyi. Tukawatuma kuwa ni wabashiri na waonyaji. Wenye kuongoka wakawaitikia, na wapotovu wakawafanyia inda! Je, watu wako wameghafilika na kweli hii? Je, wamekalishwa kitako wasiweze kutembea wakaona hao wa kale tulivyo wateketeza duniani? Na mwisho wao ni Motoni; wakaamini wenye kuamini tukawaokoa na tukawanusuru duniani. Na malipo ya Akhera ni bora kwa wenye kumkhofu Mwenyezi Mungu, wasimshirikishe wala wasimuasi. Zimeharibika akili zenu, enyi wakaidi, hata hamwezi kufikiri wala kuzingatia!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hatukuwatuma kabla yako, ewe Mtume, kwa watu isipokuwa wanaume miongoni mwao ambao tunawateremshia wahyi wetu, na wao ni miongoni mwa watu wa mijini, kwani hao wana uwezo zaidi wa kuuelewa ulinganizi na ujumbe, wawaamini wenye kuongoka kwenye haki na wawakanusha wenye kupotea njia yake. Basi si watembee katika ardhi wajionee ulikuwa vipi mwisho wa wakanushaji waliopita na ni maangamivu gani yaliyowashukia? Na malipo mema ya Nyumba ya Akhera ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani, kwa walioamini na wakamuogopa Mola wao. Basi hamfikirii mkazingatia?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net