Yusuf 12:108
يوسفقُلْ هَـٰذِهِۦ سَبِيلِىٓ أَدْعُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِى ۖ وَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Sema: Hii ndiyo njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ufahamu mzuri - mimi na wale wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, na wala mimi si katika washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina. [108]
[108] Ewe Muhammad! Wazindue mwisho wa uwezo wako, na waonyeshe hadi ya juhudi yako, uwaambie: Huu ndio Mwendo wangu na Njia yangu. Nawaita watu wafuate Njia ya Mwenyezi Mungu. Na mimi nimethibiti katika hili jambo langu, na kadhalika anayaitia hayo kila mwenye kunifuata na akaiamini sharia yangu. Na namtakasa Mwenyezi Mungu Subhanahu na kila kisicho kuwa laiki yake. Wala mimi simshirikishi Yeye na kitu chochote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, «Hii ni njia yangu, ninaita kwenye kumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake, nikiwa kwenye hoja inayotoka kwa Allah Mtukufu na uhakika, mimi na anayenifuata. Na ninamtakasa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, na washirika na mimi si katika wale wanaomshirikisha pamoja na Allah Mtukufu viumbe».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net