Yusuf 12:107
يوسفأَفَأَمِنُوٓا۟ أَن تَأْتِيَهُمْ غَـٰشِيَةٌ مِّنْ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوْ تَأْتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Je, wana amani kuwa iwajie adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au iwajie Saa ya Kiyama kwa ghafla, na hali hawatambui?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Wanaaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au haitawafikia Saa ya Kiyama kwa ghafla, na hali hawatambui?. [107]
[107] Kwani wamechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, wakadhaminika isiwapate adhabu ya kuwagubika kwa nakama yake, kama ilivyo wafanyia walio watangulia kabla yao? Au Kiyama kisiwajie kwa ghafla, kikawatesa nao wameshikamana na ushirikina na ukafiri na kisha mwisho wao uwe Motoni?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, wana chochote kinachowafanya wasalimike isiwashukie wao adhabu kutoka kwa Allah Mtukufu yenye kuwaenea au iwajie wao Siku ya Kiyama ghafla na hali wao hawatambui wala hawana hisia na hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net