Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 106

Yusuf 12:106

يوسف

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ

Maana

Na wengi wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina. [106]

[106] Na kati yao wapo wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu, wanamkubali kuwa ni Mola Mlezi, na kwamba Yeye ni Muumba wa kila kitu. Lakini imani ya wengi wao haikusimama juu ya msingi madhubuti wa Tawhid! Basi hawaukubali Upweke wa Mwenyezi Mungu kwa njia ya usafi. Lakini katika nafsi zao umo mchanganyiko wa imani unao wapelekea katika njia za washirikina, mapagani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa wenye kuzipa mgongo dalili za Allah Mtukufu hawakubali kwamba Allah Mtukufu ni Mwenye kuwaumba, ni Mwenye kuwapa riziki, ni Muumba wa kila kitu na ni Mstahiki wa kuabudiwa isipokuwa katika hali ya kumshirikisha kwa kuabudu kwao masanamu na mizimu. Allah Mtukufu Ametukuka na kutakasika na hilo kabisa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net