Yusuf 12:105
يوسفوَكَأَيِّن مِّنْ ءَايَةٍ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ يَمُرُّونَ عَلَيْهَا وَهُمْ عَنْهَا مُعْرِضُونَ
Na ni ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, lakini wao wanazipuuza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazo zipitia, na hali ya kuwa wanazipuuza. [105]
[105] Na dalili ni nyingi mno za kuonyesha kuwepo Muumba, na Upweke wake, na Ukamilifu wake, ziliomo katika mbingu na ardhi, ambazo wanaziona watu wako, na wanazipuuza kwa inda, hawataki kuzizingatia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na dalili zenye kuonyesha upweke wa Allah Mtukufu na uwezo Wake ni nyingi, zimeenea kwenye mbingu na ardhi, kama jua, mwezi, majabali na miti. Wanaziona lakini wamezipa mgongo, hawazifikirii na wala hawazingatii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net