Yusuf 12:104
يوسفوَمَا تَسْـَٔلُهُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ
Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. [104]
[104] Wala hatukusudii kwa hadithi za uwongofu unazo waeleza kuwa ndio upate malipo au manufaa. Ikiwa hawaongoki hawa usiwahuzunikie. Mwenyezi Mungu atawaongoa watu wengineo. Kwani Sisi hatukuwateremshia wao tu peke yao. Na haya si chochote ila ni mawaidha, na mazingatio kwa kila aliye umbwa na Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hutaki kwa watu wako ujira wa kuwaongoa kwenye Imani. Na yale uliyotumwa nayo ya Qur’ani na uongofu ni mawaidha kwa watu wote wanajikumbusha kwayo na wanaongoka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net