Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 99

Yusuf 12:99

يوسف

فَلَمَّا دَخَلُوا۟ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ٱدْخُلُوا۟ مِصْرَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ

Maana

Na wakati walipoingia alimokuwa Yusuf, aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akipenda) kwa amani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah, mmo katika amani. [99]

[99] Yaa'qub akasafiri kwenda Misri pamoja na ahali zake mpaka akafika huko. Walipo ingia kwa Yusuf, naye alikuwa kawapokea kwenye milango ya Misr, huruma na shauku ilimpeleka kwa haraka kwa baba na mama yake! Akawakaribisha na akawataka wao na ahali zake wakae Misri kwa amani na salama kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ya‛qûb na watu wa nyumbani kwake wakatoka kuelekea Misri wakimkusudia Yûsuf. Walipofika kwake, Yûsuf aliwakumbatia wazazi wake wawili na akawaambia (wao wote), «Ingieni Misri kwa matakwa ya Allah Mtukufu na hali mkiwa mko kwenye amani na mumeepukana na shida, ukame na kila zito».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net