Yusuf 12:98
يوسفقَالَ سَوْفَ أَسْتَغْفِرُ لَكُمْ رَبِّىٓ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Akasema: Nitakujawaombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Nitakuja kuombeeni msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kusamehe. [98]
[98] Akasema Yaa'qub nitaendelea kutaka msamaha kwa Mwenyezi Mungu kufutiwa dhambi zenu. Na hakika Yeye peke yake ndiye mwenye maghfira ya milele na rehema ya daima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ya‛qûb akasema, «Nitamuomba Mola wangu Awasamehe dhambi zenu, kwani Yeye ni Mwingi wa kusamehe dhambi za waja Wake wanaotubia, ni Mwingi wa rehema kwao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net