Yusuf 12:97
يوسفقَالُوا۟ يَـٰٓأَبَانَا ٱسْتَغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَآ إِنَّا كُنَّا خَـٰطِـِٔينَ
Wakasema: Ewe baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hakika sisi tulikuwa katika waliokosa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: ewe baba yetu, tusamehe Dhambi zetu hapana shaka sisi, tulikuwa na Makosa. [97]
[97] Hapo wakamkabili kwa kumtaka msamaha, wakimtaraji awasamehe, na awatakie kwa Mwenyezi Mungu maghfira kwa madhambi yao. Kwani wao walimhakikishia katika kule kutubu kwao kwamba wao walikuwa ni wenye kutenda madhambi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanawe wakasema, «Ewe baba yetu, tuombee Mola wako Atusamehe na Atusitiri dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa wakosa katika yale tuliyomfanyia Yûsuf na ndugu yake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net