Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 96

Yusuf 12:96

يوسف

فَلَمَّآ أَن جَآءَ ٱلْبَشِيرُ أَلْقَىٰهُ عَلَىٰ وَجْهِهِۦ فَٱرْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّىٓ أَعْلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Basi alipofika tu mbashiri huyo, akalitupa shati hilo usoni pake, basi akarejea kuona. Akasema: Je, sikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea kuona. Akasema: Je! Sikukwambieni kuwa mimi najua ya Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi? [96]

[96] Akashikilia tamaa yake akingojea rehema ya Mwenyezi Mungu, na ahali zake wakashikilia kumdhania dhana mbovu mpaka alipo fika mtu aliye chukua kanzu na kumbashiria kwamba Yusuf yupo salama salmina. Ilipo wekwa kanzu usoni kwa Yaa'qub akainusa harufu yake, moyo wake ulijaa furaha, macho yake yakarejea kuona. Yule mjumbe alipo msimulia hali ya Yusuf, na kwamba anamtaka yeye asafiri ende pamoja na ahali zake, aliwageukia walio kuwa naye akiwakumbusha ule utabiri wake, na akiwakaripia kwa vile walivyo mkadhibisha. Akawataka wakumbuke yale aliyo wahakikishia pale punde kwamba yeye anaijua rehema ya Mwenyezi Mungu na fadhila yake wasio ijua wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alipokuja mwenye kumpa bishara Ya‛qûb kwamba Yûsuf yuko hai, akaitupa kanzu ya Yûsuf usoni mwake akarudi Ya‛qûb kuwa yuaona, akajawa na furaha na akawaambia waliokuwa hapo kwake, «Je, sikuwapa habari kwamba mimi nayajua kutoka kwa Allah Mtukufu msiyoyajua ya fadhila Zake, rehema Zake na ukarimu Wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net