Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 95

Yusuf 12:95

يوسف

قَالُوا۟ تَٱللَّهِ إِنَّكَ لَفِى ضَلَـٰلِكَ ٱلْقَدِيمِ

Maana

Wakasema: Tallahi! Hakika wewe bado ungali katika upotovu wako wa zamani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Wallahi! Hakika bado ungali katika upotovu wako wa zamani. [95]

[95] Wale ahali zake wakamjibu jawabu kali wakiapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye yu ngali kuropokwa kwake na kupiswa kwake kwa uzee! Basi akajitayarisha alivyo jitayarisha kwa mapenzi yake yaliyo pita kiasi ya kumpenda Yusuf, na kuendelea kwake kumkumbuka na kutaraji kukutana naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waliohudhuria hapo kwake walisema, «Tunaapa kwa Allah Mtukufu kwamba wewe bado uko kwenye telezo lako la zamani la kumpenda Yûsuf na kwamba wewe hutamsahau».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net