Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 94

Yusuf 12:94

يوسف

وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلْعِيرُ قَالَ أَبُوهُمْ إِنِّى لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَ ۖ لَوْلَآ أَن تُفَنِّدُونِ

Maana

Na ulipoondoka tu msafara, baba yao akasema: Hakika mimi ninaipata harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ulipo ondoka tu msafara baba yao alisema: Hakika mimi nasikia harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu [94]

[94] Wakaondoka na ile kanzu. Na moyo wa Yaa'qub ulikuwa umezama kungojea nini litalo leta safari ya wanawe. Na Mwenyezi Mungu alikuwa yu pamoja naye katika kungojea huko, ikawa roho yake imeshikamana na roho zao. Basi ule msafara wao ulipo toka nchi ya Misri katika njia yake kumwendea yeye, aliwaambia ahali zake hayo kwa kusema: Mimi naihisi harufu ninayo ipenda ya Yusuf inanijaa. Na lau kuwa sikhofu kwamba mtanituhumu kwa niyasemayo ningeli kwambieni mengi ya Yusuf kuliko hizi hisiya na mawazo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Msafara ulipotoka nchi ya Misri wakiwa na ile kanzu, Ya‛qûb alisema kuwaambia wale waliokuwa na yeye, «Mimi nasikia harufu ya Yûsuf, ingawa nyinyi mtanifanya ni mchache wa akili, mtanicheza shere na mtadai kwamba maneno haya yametoka kwangu bila ya fahamu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net