Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 93

Yusuf 12:93

يوسف

ٱذْهَبُوا۟ بِقَمِيصِى هَـٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِى يَأْتِ بَصِيرًا وَأْتُونِى بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ

Maana

Nendeni na shati langu hili na mlitupe usoni mwa baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mnijie na ahali zenu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mje nao watu wenu wote wa nyumbani. [93]

[93] Kisha Yusuf akawauliza khabari za baba yao. Walipo mwambia kuwa hali yake ni mbaya na hawezi kuona kwa wingi wa hamu na majonzi, aliwapa kanzu yake, na akawaambia: Rejeeni kwa baba yangu, na hii kanzu mwekeeni usoni pake. Kwa hivyo atakuwa na yakini kuwa mimi nimo katika salama, na moyo wake utajaa furaha, na Mwenyezi Mungu atamjaalia iwe ni sababa ya kurejea kuona kwake. Hapo tena njooni naye kwangu, na ahali zenu wote pamoja.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na alipowauliza kuhusu baba yake, walimpa habari ya kupofuka macho yake kwa kumlilia. Akawaambia, «Rudini kwa baba yenu mkiwa na kanzu yangu hii, mtupieni usoni mwake na macho yake yatarudi kuona, kisha waleteni kwangu watu wenu wote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net