Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 92

Yusuf 12:92

يوسف

قَالَ لَا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ ٱلْيَوْمَ ۖ يَغْفِرُ ٱللَّهُ لَكُمْ ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ

Maana

Akasema: Leo hakuna lawama yoyote juu yenu. Mwenyezi Mungu atawasamehe, naye ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wanaorehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanao rehemu. [92]

[92] Yule Nabii mtukufu akawajibu kwa kusema: Hapana lawama kwenu leo, wala kusutana. Lenu kutoka kwangu ni msamaha ulio mwema kwa fadhila ya nasaba na haki ya udugu. Na namuomba Mwenyezi Mungu akusameheni na akughufirieni. Na Yeye ndiye Mwenye rehema kuu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yûsuf akawaambia, «Hamlaumiwi leo; Allah Mtukufu Atawasamehe. Na Yeye ni Mwenye huruma zaidi ya wenye huruma kwa anayetubia dhambi zake na akarejea kwenye utiifu Kwake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net