Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 91

Yusuf 12:91

يوسف

قَالُوا۟ تَٱللَّهِ لَقَدْ ءَاثَرَكَ ٱللَّهُ عَلَيْنَا وَإِن كُنَّا لَخَـٰطِـِٔينَ

Maana

Wakasema: Tallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa. [91]

[91] Wakasema: Uliyo sema ni kweli, na tunakuhakikishia kwa kiapo kwamba hapana shaka Mwenyezi Mungu amekutukuza kwa uchamngu, na subira, na sera njema. Na amekupa pia utawala na cheo cha juu. Na sisi hakika tulikuwa wenye kutenda dhambi kwa tuliyo kutendea wewe na nduguyo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu ametudhalilisha kwako, na ametulipa malipo ya wenye kutenda dhambi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakasema, «Tunaapa kwa Allah Mtukufu kwamba Allah Mtukufu amekutukuza juu yetu na Amekufanya bora kwa elimu, upole na utukufu, ingawa sisi ni wakosa kwa yale tuliyokufanyia wewe na ndugu yako kwa kukusudia».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net