Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 90

Yusuf 12:90

يوسف

قَالُوٓا۟ أَءِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُ ۖ قَالَ أَنَا۠ يُوسُفُ وَهَـٰذَآ أَخِى ۖ قَدْ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَآ ۖ إِنَّهُۥ مَن يَتَّقِ وَيَصْبِرْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Wakasema: Kumbe hakika wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni kaka yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anayemcha Mungu na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Kumbe wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anaye mcha Mungu na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu haachi ukapotea ujira wa wafanyao mema. [90]

[90] Kuzinduliwa huku kwa furaha kuliwatambulisha kwamba huyu ndiye Yusuf. Wakamtazama kisha wakasema kwa yakini: Hakika wewe ndiye kweli Yusuf! Na Yusuf mwenye ukarimu aliwaambia kwa kuwakubalia: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufadhili kwa kutuvua kwa salama tusihiliki, na kwa kutupa hadhi na madaraka! Na hayo yamekuwa ni malipo ya Mwenyezi Mungu kwa usafi wangu na wema wangu. Na hakika Mwenyezi Mungu haachi ukapotea ujira wa mtendaji mema na akaendelea nao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakasema, «Je, wewe ni Yûsuf?» Akasema, «Ndio. Mimi ni Yûsuf na huyu ni ndugu yangu. Allah Mtukufu Ametukirimu, akatukusanya pamoja baada ya kutengana. Hakika Mwenye kumcha Allah Mtukufu na akavumilia shida, Allah Mtukufu hamuondolei malipo ya wema wake, Hakika atamlipa malipo mema zaidi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net