Yusuf 12:89
يوسفقَالَ هَلْ عَلِمْتُم مَّا فَعَلْتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذْ أَنتُمْ جَـٰهِلُونَ
Akasema: Je, mnajua yale mliyomfanyia Yusuf na kakaye mlipokuwa wajinga?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Je! Mmejua mliyo mfanyia Yusuf na nduguye mlipo kuwa wajinga? [89]
[89] Yusuf akaingiwa na huruma ya udugu ambayo inasamehe maovu. Akaanza kuwafunulia khabari zake kwa kuwaambia kwa lawama: Je! Mmejua ule uovu mlio mfanyia Yusuf kwa kumtumbukiza kisimani, na maudhi mlio mfanyia nduguye, mkafanya hayo kwa ujinga ulio kusahaulisheni huruma na udugu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Aliposikia maneno yao alilainika juu yao, akajitambulisha kwao na akasema, «Je, mnayakumbuka mabaya mliyomfanyia Yûsuf na ndugu yake mlipokuwa katika hali ya kutojua vile matendo yenu yataishia?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net