Yusuf 12:88
يوسففَلَمَّا دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ قَالُوا۟ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْعَزِيزُ مَسَّنَا وَأَهْلَنَا ٱلضُّرُّ وَجِئْنَا بِبِضَـٰعَةٍ مُّزْجَىٰةٍ فَأَوْفِ لَنَا ٱلْكَيْلَ وَتَصَدَّقْ عَلَيْنَآ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَجْزِى ٱلْمُتَصَدِّقِينَ
Basi walipoingia alimokuwa Yusuf, wakasema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida kubwa, sisi na ahali zetu. Na tumekujia na mali kidogo. Basi tutimizie tu kipimo na tupe sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi walipo ingia kwa Yusuf walisema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida, sisi na watu wetu. Na tumeleta mali kidogo. Basi tupimie kipimo na fanya kama unatupa sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka. [88]
[88] Nduguze Yusuf walimwitikia baba yao kwa matakwa yake. Wakatoka kwenda Misri, na wakajaribu kukutana na mtawala wake ambaye baadae ikadhihiri kuwa ndiye Yusuf! Walipo ingia kwake walisema: Ewe Mheshimiwa! Sisi na watu wetu tumepata shida ya njaa na madhara ya mwili na nafsi. Na tumekuletea mali chache ndio bidhaa yetu. Nayo ni ya kukataliwa kwa kuwa ni kidogo na mbaya, wala haitoshi kwa hayo tunayo taraji kwako. Lakini sisi tunataraji kwako utupimie kwa ukamilifu na utacho tuzidishia kiwe ni sadaka unayo tupa. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huwalipa wenye kutoa sadaka thawabu njema kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakaenda Misri. Na walipoingia kwa Yûsuf walisema, «Ewe kiongozi, tumepatikana na ukame na ukavu, na tumekujia na thamani isiyokuwa nzuri na iliyo chache, basi tupe kwa hii thamani kiasi ulichokuwa ukitupa kabla kwa thamani nzuri. Na ututunuku kwa kukubali kupokea thamani hii mbaya iliyo chache, na utulegezee juu ya hiyo thamani, hakika Allah Mtukufu Anawalipa wema wale wenye kuwasaidia wahitaji kwa mali zao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net