Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 87

Yusuf 12:87

يوسف

يَـٰبَنِىَّ ٱذْهَبُوا۟ فَتَحَسَّسُوا۟ مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَا۟يْـَٔسُوا۟ مِن رَّوْحِ ٱللَّهِ ۖ إِنَّهُۥ لَا يَا۟يْـَٔسُ مِن رَّوْحِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْقَوْمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ

Maana

Enyi wanangu! Nendeni mumtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri. [87]

[87] Na kuwa na imani na Mwenyezi Mungu ndio huhuisha matumaini. Kwa hivyo zile dhiki za moyo hazikuondoka kwa matarajio ya Yaa'qub kumrudia wanawe, na yakamtia katika moyo wake kuwa wangali wahai, na kwamba wakati wa kukutana nao ndio umefika. Akawaamrisha wanawe wende wakawatafute, akawaambia: Enyi wanangu! Rejeeni Misri muwe na kaka yenu, na mumtafute Yusuf na nduguye, muulize khabari zao kwa upole bila ya watu kujua. Wala msikate tamaa kwa Mwenyezi Mungu kuturehemu kwa kuwarudisha. Kwani hawakati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa wale wanao kanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ya‛qûb akasema, «Enyi wanangu! Rudini Misri mpeleleze habari za Yûsuf na ndugu yake, wala msikate tamaa na rehema za Allah Mtukufu, kwani hawakati tamaa na rehema za Allah Mtukufu isipokuwa wenye kuukanusha uwezo Wake, wenye kumkataa Yeye».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net