Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 86

Yusuf 12:86

يوسف

قَالَ إِنَّمَآ أَشْكُوا۟ بَثِّى وَحُزْنِىٓ إِلَى ٱللَّهِ وَأَعْلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu tu sikitiko langu na huzuni wangu. Na ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu. Na ninajua kwa Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi. [86]

[86] Maneno yao hayakumuathiri hata chembe. Akawajibu kwa kusema: Mimi sikukushitakieni, wala sikukutakeni mnipunguzie machungu yangu! Mimi sina ila Mwenyezi Mungu tu wa kumnyenyekea na kumshitakia dhiki zangu nzito na nyepesi. Wala siwezi kumficha hayo wala lolote nisilo liweza, kwani mimi natambua wema wake wa kutenda na ukunjufu wa rehema yake, jambo ambalo nyinyi hamlijui!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ya‛qûb akasema kuwajibu, «Simuonyeshi hamu yangu na masikitiko yangu isipokuwa Allah Mtukufu Peke Yake. Yeye Ndiye Mwenye kuondoa shida na matatizo. Na ninayajua, kuhusu rehema za Allah Mtukufu na maliwazo Yake, mambo msiyoyajua».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net