Yusuf 12:85
يوسفقَالُوا۟ تَٱللَّهِ تَفْتَؤُا۟ تَذْكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوْ تَكُونَ مِنَ ٱلْهَـٰلِكِينَ
Wakasema: Tallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa sana au uwe katika walioangamia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Wallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe katika walio hiliki. [85]
[85] Siku zikapita na Yaa'qub kazama katika majonzi yake. Wanawe wakaogopa isije kuwa khatari. Wakamkabili kumtaka apunguze huzuni yake, nao wako baina ya kumwonea huruma na kuchukia kuwa bado yu ngali akimkumbuka Yusuf wakamwambia: Kama hukujipunguzia nafsi yako hapana shaka kumkumbuka Yusuf kutakuzidishia machungu yako yakukondeshe mpaka ukaribie kufa, au ufe khasa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanawe wakasema, «Tunaapa kwa Allah Mtukufu, utaendelea kumkumbuka Yûsuf na kuwa na huzuni nyingi juu yake mpaka ukaribie kuangamia au uangamie kikweli, basi ipumzishe nafsi yako».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net