Yusuf 12:84
يوسفوَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَـٰٓأَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَٱبْيَضَّتْ عَيْنَاهُ مِنَ ٱلْحُزْنِ فَهُوَ كَظِيمٌ
Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Huzuni wangu mkubwa juu ya Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kutokana na huzuni, na akaizuia bila ya kuidhirisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Masikini Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kwa huzuni aliyo kuwa akiizuia. [84]
[84] Akadhikika kwa waliyo yasema, akajitenga nao, kashughulika na msiba wake na huzuni kumkosa Yusuf. Macho yake yakafanya kiza kwa wingi wa huzuni, naye akiificha sana. Huzuni kubwa huleta ugonjwa wa macho unao itwa GLOKOMA, na weupe huzidi mpaka mtu mwisho anakuwa kipofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ya‛qûb akawapa mgongo na asishughulike nao, ukiwa moyo wake umeingia dhiki kwa maneno waliyoyasema, na akasema, «Ewe hasara yangu juu ya Yûsuf!» Na macho yake yakawa meupe, kwa kuondoka weusi wake kwa masikitiko mengi. Moyo wake umejaa huzuni tele, lakini alikuwa akiificha sana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net