Yusuf 12:100
يوسفوَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى ٱلْعَرْشِ وَخَرُّوا۟ لَهُۥ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَـٰٓأَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُءْيَـٰىَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّى حَقًّا ۖ وَقَدْ أَحْسَنَ بِىٓ إِذْ أَخْرَجَنِى مِنَ ٱلسِّجْنِ وَجَآءَ بِكُم مِّنَ ٱلْبَدْوِ مِنۢ بَعْدِ أَن نَّزَغَ ٱلشَّيْطَـٰنُ بَيْنِى وَبَيْنَ إِخْوَتِىٓ ۚ إِنَّ رَبِّى لَطِيفٌ لِّمَا يَشَآءُ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْحَكِيمُ
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi, na wote wakaporomoka kumsujudia. Akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Mola wangu Mlezi ameifanya kuwa kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia uzuri kunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani baada ya Shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Na Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia wema kunitoa gerezani, na kukuleteni kutoka jangwani baada ya Shet'ani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Bila ya shaka Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima. [100]
[100] Msafara ukenda ndani ya nchi ya Misri mpaka ukafika kwenye nyumba ya Yusuf. Wakaingia, na Yusuf akawatanguliza wazazi wake akawaweka kwenye kochi. Yaa'qub na ahali zake wakajaa furaha kwa uzuri wa mapokezi aliyo watengezea Mwenyezi Mungu katika mikono ya Yusuf. Kwani kwa hayo ukoo wote umekusanyika hapo baada ya mfarakano, na umetukuka makamu makubwa ya utukufu na hishima. Wakamuamkia maamkio yaliyo zowewa na watu tangu zamani ya kuwaamkia maraisi na watawala. Wakaonyesha unyenyekevu kwa utawala wake. Yale yalimkumbusha Yusuf ile ndoto yake ya utotoni. Akamwambia baba yake: Hii ndio tafsiri ya ndoto niliyo iota na nikakusimulia ya kwamba nimeota usingizini kuwa nyota kumi na moja na jua na mwezi zinanisujudia; ni hivi basi Mola wangu Mlezi ameitimiza, na amenitukuza na amenifanyia hisani. Amedhihirisha kuwa sina makosa, na akanitoa kifungoni, na akakuleteni kutoka jangwani tukutane, baada ya Shetani kutufisidi baina yangu na ndugu zangu, akawachochea dhidi yangu. Na haya yote yasinge kuwa bila ya Mwenyezi Mungu kuyafanya. Yeye ndiye wa kupanga na kuyafanya mambo yatimie kama atakavyo. Na Yeye ndiye Mwenye kuzunguka kila kitu kwa ujuzi wake, ambaye hukumu yake ni yenye kushinda katika kila jambo na kadhiya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akawakalisha wazazi wake wawili kwenye kitanda cha ufalme wake kwa njia ya kuwatukuza. Na wazazi wake na ndugu zake kumi na moja wakamsalimia kwa kumuinamia kwa kumwamkia na kumtukuza na sio kumuabudu na kumnyenyekea. Na hilo lilikuwa linaruhusiwa katika Sheria yao, na limeharamishwa katika Sheria yetu, kwa ajili ya kuziba njia inayopelekea kwenye ushirikina. Na Yûsuf akamwambia baba yake, «Kusujudu huku ndio tafsiri ya ndoto yangu niliyokusimulia kabla, katika udogo wangu, Allah Mtukufu Ameifanya ni kweli. Na amenifadhili aliponitoa jela na akawaleta nyinyi kutoka jangwani, baada ya Shetani kuharibu uhusiano wa undugu baina yangu mimi na ndugu zangu. Hakika Mola wangu ni Mpole wa kupitisha Analolitaka. Yeye Anayajua sana maslahi ya waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net