Yusuf 12:101
يوسفرَبِّ قَدْ ءَاتَيْتَنِى مِنَ ٱلْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِى مِن تَأْوِيلِ ٱلْأَحَادِيثِ ۚ فَاطِرَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ أَنتَ وَلِىِّۦ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِى مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّـٰلِحِينَ
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa katika ufalme, na umenifunza katika tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na niunganishe na walio wema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema. [101]
[101] Yusuf akamwelekea Mwenyezi Mungu akimshukuru kwa kuzihisabu neema zake juu yake, na akimwomba amzidishie fadhila zake, kwa kusema: Ewe Mola wangu Mlezi! Neema zako kwangu ni nyingi mno, na bora mno! Umenipa utawala, na nakuhimidi kwa hayo. Ukanitunukia ilimu ya kufasiri ndoto kama ulivyo nitunukia! Ewe Muumba mbingu na ardhi! Wewe ndiye uliye miliki mambo yangu yote, na Mtawala wa neema za uhai wangu na baada ya kufa kwangu! Nifungamanishe nawe kwa ulivyo waridhia Manabii wako katika Dini ya Kiislamu, na uniingize katika kundi la ulio waongoa kwenye wema miongoni mwa baba zangu, na waja wako walio wema, walio safika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha Yûsuf alimuomba Mola wake akisema, «Mola wangu! Umenipa Ufalme wa Misri, na umenifundisha kutafsiri ndoto na elimu nyinginezo. Ewe Muumba, na Mtengenezaji, mbingu na ardhi! Wewe Ndiye Msimamizi wa mambo yangu ulimwenguni na Akhera. Nifishe unichukue kwako nikiwa Muislamu na unikutanishe na waja wako wema miongoni mwa Manabii watenda mema na walioteuliwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net