Yusuf 12:102
يوسفذَٰلِكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۖ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ أَجْمَعُوٓا۟ أَمْرَهُمْ وَهُمْ يَمْكُرُونَ
Hizo ni katika habari za ghaibu tulizokufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipoazimia jambo lao hilo walipokuwa wanafanya njama zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipo azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua vitimbi. [102]
[102] Ewe Nabii! Haya tuliyo kusimulia ni katika khabari zilizo pita za kale. Hazikukufikia ila kwa wahyi ulio toka kwetu. Wala wewe hukuwapo pale nduguze Yusuf walipo kuwa wakipanga njama. Wala wewe hukuwa unavijua vitimbi vyao ila kwa kusimuliwa nasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hayo yaliyotajwa ya habari za Yûsuf ni miongoni mwa habari za ghaibu, tunakuelezea, ewe Mtume, kwa njia ya wahyi. Na hukuwako pamoja na ndugu zake Yûsuf walipompangia kumtia kisimani na wakamfanyia hila yeye na baba yake. Hii inaonesha dalili ya ukweli wako na kwamba Allah Mtukufu Anakuletea wahyi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net