Yusuf 12:82
يوسفوَسْـَٔلِ ٱلْقَرْيَةَ ٱلَّتِى كُنَّا فِيهَا وَٱلْعِيرَ ٱلَّتِىٓ أَقْبَلْنَا فِيهَا ۖ وَإِنَّا لَصَـٰدِقُونَ
Na uliza mji tuliokuwamo, na msafara tuliokuja nao. Na hakika sisi ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na waulize watu wa mji tulio kuwako, na msafara tulio kuja nao. Na hakika sisi tunasema kweli. [82]
[82] Na ikiwa wewe una shaka na haya tunayo kwambia mtume mtu akuletee ushahidi wa watu wa Misri. Na pia wewe mwenyewe waulize wasafiri wenzetu tulio rudi nao, ipate kudhihiri kuwa sisi hatuna lawama. Nasi tunakuhakikishia kuwa sisi ni wakweli katika haya tuyasemayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waliporejea, wakampa habari baba yao yaliyotokea na wakamtaka ahakikishe yale waliyomwambia wakisema, «Na waulize, ewe baba yetu, watu wa Misri na wale waliokuwa pamoja na sisi kwenye msafara tuliorudi nao. Na sisi ni wakweli kwa yale tuliyokusimulia».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net