Yusuf 12:81
يوسفٱرْجِعُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَبِيكُمْ فَقُولُوا۟ يَـٰٓأَبَانَآ إِنَّ ٱبْنَكَ سَرَقَ وَمَا شَهِدْنَآ إِلَّا بِمَا عَلِمْنَا وَمَا كُنَّا لِلْغَيْبِ حَـٰفِظِينَ
Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba. Na sisi hatutoi ushahidi isipokuwa kwa tunayoyajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Mwanao ameiba. Na sisi hatutoi ushahidi ila kwa tunayo yajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu. [81]
[81] Rejeeni nyinyi kwa baba yenu, na msimulieni kisa chote hichi. Na mwambieni: Mkono wa mwanao ulikunjuka akakiiba kikopo cha mfalme, na kimekutikana katika bahasha yake. Kwa huo wizi wake ndio ameshikwa. Nasi hatukwambii ila tuliyo yaona, na wala sisi hatukuwa tunajua yaliyo fichikana katika hukumu ya Mwenyezi Mungu pale tulipo kutaka nawe ukatupa tumhifadhi na turejee naye kwako kama tulivyo ahidiana na tukafungana. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa uadilifu kuliko mahakimu wote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Rudini nyinyi kwa baba yenu, mpeni habari ya yaliyojiri na mwambieni, «Mwanao Binyãmîn ameiba, na hatukushuhudia isipokuwa kwa lile ambalo tuna uhakika nalo. Kwani tumekiona kipimio kwenye mzigo wake, na hatukuwa na ujuzi wa ghaibu kuwa yeye ataiba tulipokuahidi kumrudisha».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net