Yusuf 12:80
يوسففَلَمَّا ٱسْتَيْـَٔسُوا۟ مِنْهُ خَلَصُوا۟ نَجِيًّا ۖ قَالَ كَبِيرُهُمْ أَلَمْ تَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ أَبَاكُمْ قَدْ أَخَذَ عَلَيْكُم مَّوْثِقًا مِّنَ ٱللَّهِ وَمِن قَبْلُ مَا فَرَّطتُمْ فِى يُوسُفَ ۖ فَلَنْ أَبْرَحَ ٱلْأَرْضَ حَتَّىٰ يَأْذَنَ لِىٓ أَبِىٓ أَوْ يَحْكُمَ ٱللَّهُ لِى ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْحَـٰكِمِينَ
Basi walipokata tamaa naye, wakaenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua agano kutoka kwenu kwa Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo namna mlivyokosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitatoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa wanaohukumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walipo kata tamaa naye wakenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kwenu kutokana na Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo mlimkosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitotoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu. [80]
[80] Ilipo katika tamaa yao, wakavunjika moyo kukubaliwa maombi yao, wakenda pembeni peke yao wakishauriana juu ya msimamo wao na baba yao. Ilipo ishia shauri kwa mkubwa wao mwenye kupanga mambo yao, aliwaambia: Haikufalieni kuisahau ahadi ya kiapo mliyo mpa baba yenu ya kuwa mtamhifadhi ndugu yenu mpaka mrudi naye, wala mlivyo fungana naye kabla yake kuwa mtamlinda Yusuf, na hayo mkayavunja! Kwa hivyo mimi nitabaki Misri wala sitotoka ila afahamu baba yetu ukweli wa hali hii, na akaniachilia nirejee kwake, au Mwenyezi Mungu anihukumie kurejea kwa hishima, na akanisahilishia njia kwa sababu yoyote ile. Na Yeye ndiye Mbora wa uadilifu kuliko mahakimu wote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walipokata tamaa ya kukubali kwake matakwa yao, walikaa kando na watu wakawa wanashauriana baina yao. Mkubwa wao kimiaka alisema, Je hamjui kuwa baba yenu alichukuwa kwenu ahadi ya mkazo kuwa mtamrudisha ndugu yenu mpaka mshindwe, Na kabla ya tukio hili mlifanya kasoro kuhusu Yûsuf na mkamzungukia kinyume kwa hiana. Kwa hivyo sitaondoka kwenye ardhi ya Misri mpaka baba yangu aniamuru niondoke au Mola wangu Anihukumie niondoke na niweze kumchukua ndugu yangu. Na Allah Mtukufu ni Bora wa wanaohukumu na ni muadilifu zaidi wa wenye kutoa uamuzi baina ya watu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net