Yusuf 12:79
يوسفقَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ أَن نَّأْخُذَ إِلَّا مَن وَجَدْنَا مَتَـٰعَنَا عِندَهُۥٓ إِنَّآ إِذًا لَّظَـٰلِمُونَ
Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu. Hakika, hapo tutakuwa ni wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipo kuwa tuliye mkuta naye kitu chetu. Hivyo basi tutakuwa wenye kudhulumu. [79]
[79] Wala haikufalia kwa Yusuf kuvunja mpango alio mkubalia Mwenyezi Mungu, na kumwachia nduguye atoke mkononi mwake. Kwa hivyo maombi yao hayakumlainisha kitu. Akawajibu jawabu mkato, kwa kuwaambia: Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu isije nafsi yangu ikadhulumu kwa kumzuia yeyote yule isipo kuwa yule yule tuliye mkuta nayo mali yetu. Tukimchukua mwenginewe kwa kumuadhibu tutakuwa katika hao walio vuka mipaka kwa kumshika asiye na makosa kwa madhambi ya mwovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yûsuf akasema, «Tunaomba hifadhi ya Allah Mtukufu na himaya Yake, tusiwe ni wenye kumchukua yoyote isipokuwa yule ambaye tulipata kipimio chetu kwake, kama mlivyoamua wenyewe. Kwani sisi tukifanya hayo ambayo mnataka tutakuwa ni miongoni mwa wanaohesabiwa kuwa ni waonevu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net