Yusuf 12:78
يوسفقَالُوا۟ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْعَزِيزُ إِنَّ لَهُۥٓ أَبًا شَيْخًا كَبِيرًا فَخُذْ أَحَدَنَا مَكَانَهُۥٓ ۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلْمُحْسِنِينَ
Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wema. [78]
[78] Wakawa hawana budi kujaribu kumvua ndugu yao au kumtolea fidia kwa kutaka kutimiza ile ahadi yao waliyo mpa Yaa'qub. Wakaingia kutaka kumlainisha moyo Yusuf kwa kumtajia uzee wa baba yao, wakamwambia: Ewe Mheshimiwa! Huyu ndugu yetu ana baba mtu mzima sana. Basi mfanyie huruma umchukue mmoja wetu mwenginewe awe badala ya mwanawe huyu ambaye ndiye anaye mpenda moyoni mwake. Matarajio yetu ni kuwa utatukubalia mambo yetu. Kwenu tumekwisha ona tabia yako ya ukarimu, na tumehakikisha mwendo wako wa kupenda kufanya hisani na kutenda mema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema kwa njia ya kubembeleza na kutaka kuhurumiwa ili watekeleze ahadi ya baba yao, «Ewe kiongozi, hakika yeye ana mzazi wa kiume mkubwa wa miaka anayempenda na asiyeweza kuwa mbali na yeye. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala ya Binyãmîn. Sisi tunakuona ni miongoni mwa watenda wema kwa vile unavotutendea sisi na wasiokuwa sisi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net