Yusuf 12:77
يوسفقَالُوٓا۟ إِن يَسْرِقْ فَقَدْ سَرَقَ أَخٌ لَّهُۥ مِن قَبْلُ ۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ فِى نَفْسِهِۦ وَلَمْ يُبْدِهَا لَهُمْ ۚ قَالَ أَنتُمْ شَرٌّ مَّكَانًا ۖ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا تَصِفُونَ
Wakasema: Akiwa ameiba huyu, basi hakika kakaye vile vile aliiba hapo zamani. Lakini Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao. Akasema: Nyinyi ndio mko katika pahali paovu zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ikiwa huyu ameiba, basi nduguye vile vile aliiba zamani. Lakini Yusuf aliyaweka siri moyoni mwake wala hakuwaonyesha. Akawaambia: Nyinyi mko katika hali mbaya zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayo singizia. [77]
[77] Kule kugunduliwa kikopo katika mzigo wa ndugu yake kwa ghafla kuliwashangaza nduguze na kukawababaisha. Kwa hivyo wakataka kujivua kuwa wao wote hawana makosa ila huyo na Yusuf, na kusema kuwa tabia ya wizi wameirithi kwa mama yao. Wakasema: Si ajabu kuwa huyo kaiba, kwani nduguye khalisa aliwahi kwiba vile vile! Na Yusuf akatambua kijembe chao wanacho mpigia, na yakamuudhi hayo. Lakini aliyaficha, na akawawekea jawabu moyoni mwake lau kuwa amesema wazi jawabu yenyewe inge kuwa hivi: Nyinyi mko katika hali ovu zaidi, na nyinyi ni duni zaidi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, na kutambua ukweli wa maneno yenu ya kumsingizia nduguye fedheha ya wizi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema ndugu zake Yûsuf, iwapo huyu yuwaiba, ametangulia ndugu yake kuiba (wakimaanisha Yûsuf, amani imshukie). Yûsuf akalificha hilo alilosikia la uzushi kutoka kwao ndani ya nafsi yake,na akauzungumzia moyo wake kwa kusema, «Nyinyi ni wabaya zaidi wa mahali kuliko huyo Mliyemtaja, mliponifanyia njama zile zilizokua kutoka kwenu. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi zaidi wa sifa za urongo na uzushi mnazozitoa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net