Yusuf 12:76
يوسففَبَدَأَ بِأَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَآءِ أَخِيهِ ثُمَّ ٱسْتَخْرَجَهَا مِن وِعَآءِ أَخِيهِ ۚ كَذَٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ ۖ مَا كَانَ لِيَأْخُذَ أَخَاهُ فِى دِينِ ٱلْمَلِكِ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَـٰتٍ مَّن نَّشَآءُ ۗ وَفَوْقَ كُلِّ ذِى عِلْمٍ عَلِيمٌ
Basi akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa kakaye. Kisha akalitoa katika mzigo wa kakaye. Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf. Hakuwa ni wa kumzuia kakaye kwa sheria ya mfalme huyo isipokuwa Mwenyezi Mungu akitaka. Tunamuinua daraja tumtakaye. Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi. [76]
[76] Shauri ikaishia ipekuliwe mizigo, na ikawa lazima kufanya mambo baraabara ili isionekane kuwa kuna mpango ulio pangwa. Yusuf mwenyewe ndiye aliye fanya uchunguzi, baada ya kwisha tengeza mambo. Akaanza kupekua mizigo ya wale ndugu kumi, kisha ndio akaingia kuupekua mzigo wa nduguye. Humo akakitoa kile kikopo, na kwa hivyo hila yake ikafuzu. Akawa na haki kwa hukumu ya nduguze kumshika Bin-yamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyo mpangia mambo Yusuf. Hakuwa anaweza yeye kumshika nduguye kwa mujibu wa sharia ya mfalme wa Misri tu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Naye alitaka. Basi tulimpangia mambo Yusuf, na tukamwezesha kuzirekibisha sababu na mipango baraabara na hila nzuri. Na haya ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu, ambaye humtukuza katika vyeo vya ujuzi amtakaye. Na juu ya kila mwenye ilimu yupo mwenye kumzidia katika ujuzi!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
wakarudi na ndugu zake Yûsuf kwake, akasimama mwenyewe kupekua mizigo yao. Akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake, ili kuimarisha mpango wake wa kumfanya ndugu yake abakie pamoja na yeye, kisha akamalizikia kwenye vyombo vya ndugu yake na akakitoa chombo humo. Hivyo ndivyo tulivyomsahilishia Yûsuf mpango huu ambao ulimpelekea kumchukua ndugu yake kwenye mamlaka ya mfalme wa Misri. Kwani si katika dini yake kummiliki mwizi, isipokuwa kwamba matakwa ya Allah Mtukufu yamepelekea mipango hii na kutaka uamuzi kwenye sheria ya ndugu zake Yûsuf yenye hukumu ya mwizi kufanywa mtumwa. Tunawainua daraja tunaowataka ulimwenguni juu ya wengine kama vile tulivyomuinua Yûsuf daraja. Na juu ya kila mwenye ujuzi kuna mjuzi zaidi kuliko yeye, mpaka ujuzi ukome kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, Mjuzi wa yaliyofichika na yanayoonekana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net