Yusuf 12:75
يوسفقَالُوا۟ جَزَٰٓؤُهُۥ مَن وُجِدَ فِى رَحْلِهِۦ فَهُوَ جَزَٰٓؤُهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلظَّـٰلِمِينَ
Wakasema: Malipo yake ni kwamba yule ambaye litapatikana katika shehena lake, basi huyo ndiye malipo yake. Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Malipo yake ni yule ambaye ataonekana nalo yeye huyo ndiye malipo yake. Hivi ndivyo tunavyo walipa madhaalimu. [75]
[75] Na kwa kuwa wana wa Yaa'qub walikuwa na yakini kuwa wao hawakukiba kile kikopo walisema bila ya kusitasita: Malipo ya mwenye kuchukua hicho kikopo ni kushikwa huyo na afanywe mtumwa. Ndio hivi sisi tunavyo walipa wenye kudhulumu wakachukua mali ya watu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ndugu zake Yûsuf wakasema, «Malipo ya mwizi ni kwamba yule ambaye kitapatikana kilichoibiwa kwenye mzigo wa ngamia wake basi yeye ndiye malipo yake.» Yaani atakabidhiwa, kwa sababu ya wizi wake, kwa yule aliyemuibia awe mtumwa kwake. Malipo mfano huu, nayo ni ya kufanywa mtumwa, tunawalipa wenye kufanya dhuluma kwa kuiba. Hii ndiyo dini yetu na mwendo wetu kuhusu wezi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net