Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 74

Yusuf 12:74

يوسف

قَالُوا۟ فَمَا جَزَٰٓؤُهُۥٓ إِن كُنتُمْ كَـٰذِبِينَ

Maana

Wakasema: Basi malipo yake ni nini ikiwa nyinyi ni waongo?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Basi malipo yake yatakuwa nini ikiwa nyinyi ni waongo. [74]

[74] Na Yusuf alikwisha waamrisha wafwasi wake wawaache nduguze waamue nini malipo anayo stahiki kupata yule atakaye onekana nacho kile kikopo, ili apate kumchukua nduguye kwa hukumu yao wenyewe, na iwe hukumu yao ndiyo ya kukata shauri, isiwepo njia ya kumwombea. Basi watu wa Yusuf wakawaambia wale nduguze: Nini malipo ya wevi kwenu wanapo gundulikana ni katika nyinyi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale waliopewa jukumu la kukitafuta kipimio walisema kuwaambia ndugu zake Yûsuf, «Ni ipi adhabu ya mwizi kwenu nyinyi, iwapo nyinyi ni warongo katika kauli yenu: ‘sisi si wezi’?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net