Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 73

Yusuf 12:73

يوسف

قَالُوا۟ تَٱللَّهِ لَقَدْ عَلِمْتُم مَّا جِئْنَا لِنُفْسِدَ فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا كُنَّا سَـٰرِقِينَ

Maana

Wakasema: Tallahi! Hakika mlikwishajua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Wallahi! Mnajua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi. [73]

[73] Nduguze Yusuf wakasema: Hakika kututuhumu sisi kwa wizi ni jambo la ajabu mno! Na tunahakikisha kwa kiapo ya kwamba nyinyi wenyewe mmeona katika mwendo wetu na tunavyo ishika dini yetu katika mara mbili tulipo kuja hapa kuwa mmejua yakini kuwa sisi hatutaki kuleta uharibifu katika nchi yenu. Wala si katika tabia yetu kuwa ni wezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ndugu zake Yûsuf wakasema, «Tunaapa kwa Allah Mtukufu, nyinyi mna uhakika kwa mliyoyashuhudia kutoka kwetu kwamba sisi hatukuja nchi ya Misri kufanya uharibifu, na si katika sifa zetu kuwa wezi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net