Yusuf 12:72
يوسفقَالُوا۟ نَفْقِدُ صُوَاعَ ٱلْمَلِكِ وَلِمَن جَآءَ بِهِۦ حِمْلُ بَعِيرٍ وَأَنَا۠ بِهِۦ زَعِيمٌ
Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na atakayenijia nalo, atapewa shehena nzima abebayo ngamia. Nami ni mdhamini juu ya hilo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na ataye lileta atapewa shehena nzima ya ngamia. Nami ni dhaamini wa hayo. [72]
[72] Wale wasaidizi wakajibu: Tunatafuta kikopo, nacho ni chombo anacho nywea mwenyewe mfalme. Na malipo yake kwa mwenye kukileta ni shehena nzima ya chakula anayo ibeba ngamia. Yule mkubwa wao alitilia mkazo hayo kwa kusema: Na mimi ninadhamini kutimiza ahadi hii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yule aliyeita na waliokuwa na yeye walisema, «Tumekikosa kipimio ambacho mfalme anapimia nacho. Na zawadi za mwenye kukileta ni twesha ya ngamia mmoja ya chakula.» Na yule aliyeita akasema, «Na mimi naidhamini na kuitolea ahadi hiyo twesha ya ngamia ya chakula».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net