Yusuf 12:69
يوسفوَلَمَّا دَخَلُوا۟ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيْهِ أَخَاهُ ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَنَا۠ أَخُوكَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Na walipoingia alimokuwa Yusuf, alimkumbatia kakaye na akasema: Mimi hakika ndiye yule kaka yako. Basi usihuzunike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walipo ingia kwa Yusuf alimchukua nduguye akasema: Mimi hakika ni nduguyo. Basi usihuzunike kwa waliyo kuwa wakiyafanya. [69]
[69] Walipo ingia kwa Yusuf aliwapokea kwa hishima, na khasa yule nduguye kwa baba na mama ndio akamchukua na akampa siri kwa kumwambia: Usitie shaka mimi ni nduguyo Yusuf. Basi usihuzunike kwa waliyo kufanyia wewe na waliyo nifanyia mimi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walipoingia ndugu zake Yûsuf kwake, katika nyumba yake ya kukaribisha wageni, wakiwa pamoja na ndugu yake wa kwa baba na mama, Yûsuf alimkumbatia nduguye wa kwa baba na mama na akamwambia kwa siri, «Mimi ni ndugu yako. Basi usihuzunike wala usiingiwe na dhiki kwa yale waliyonifanyia kipindi kilichopita.» Na akamuamuru alifiche jambo hilo kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net