Yusuf 12:70
يوسففَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ جَعَلَ ٱلسِّقَايَةَ فِى رَحْلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا ٱلْعِيرُ إِنَّكُمْ لَسَـٰرِقُونَ
Na alipokwishawatayarishia mahitaji yao, akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa kakaye huyo, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi msafara! Hakika nyinyi ni wezi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na alipo kwisha watengenezea mahitaji yao akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mnadi akanadi: Enyi wasafiri! Hapana shaka nyinyi ni wezi! [70]
[70] Basi baada ya kuwakirimu kwa kuja kwao, na kuwapimia chakula, na kuwazidishia shehena ya nduguye, aliwafungia mizigo yao kwa ajili ya safari. Tena akawaamrisha wasaidizi wake watumbukize chombo cha kunywea katika mzigo wa Bin-yamini. Kisha mmoja wa wasaidizi wa Yusuf alinadi: Enyi wasafiri! Ngojeni! Nyinyi ni wezi!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na alipowatayarishia Yûsuf na akawabebesha chakula ngamia wao, aliwaamuru watumishi wake wakakiweka kile chombo, ambacho alikua akiwapimia nacho watu, kwenye vyombo vya ndugu yake Binyãmîn kwa namna ambayo asitambue yoyote. Basi walipopanda kwenda zao, aliita mwenye kuita akisema, «Enyi wenye ngamia waliobebeshwa chakula, nyinyi ni wezi!»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net